In Summary

• Ojaamong alitoa tamko hilo mbele ya Rais William Ruto katika Shule ya Msingi ya Machakus.

Gavana wa Busia anaeondoka Jospeter Odeke Ojamoo

Aliyekuwa gavana wa Busia Sospeter Ojaamong amejiunga na UDA.

Ojaamong alitoa tamko hilo mbele ya Rais William Ruto katika Shule ya Msingi ya Machakus.

Ruto yuko Teso kuhudhuria mkutano wa maombi ya madhehebu mbalimbali pamoja na kuzindua miradi ya maendeleo kabla ya kuhutubia mikutano ya hadhara katika mji wa Malaba na Angurai.

Ojaamong wakati wa tamko hilo alisema kufanya kazi chini ya serikali ni uamuzi bora kuliko kiongozi yeyote anaweza kufanya.

"Kuanzia leo nimejiunga na UDA na ninatarajia kuwa serikalini kikamilifu," Ojaamong alisema.

"Njia bora ya kupata miradi bora ya maendeleo ni kwa kuunga mkono serikali."

Ojaamong amekuwa mwanachama shupavu wa ODM na mfuasi wa kinara wa ODM Raila Odinga baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Amagoro kwa mihula miwili kabla ya kuchaguliwa kuwa gavana kwa mihula mingine miwili.

Alipokuwa kwenye siasa za uchaguzi, alikuwa mwanachama wa maisha hadi wiki mbili zilizopita alipodokeza kuwa huenda akajiunga na UDA.

Waziri wa Michezo Ababu Namwamba alimpongeza Ojaamong kwa uamuzi aliofanya wa kuachana na ODM.

"Mheshimiwa Ojaamong amefanya uamuzi mzuri. Tumuunge mkono anapojiunga na nyumba ya UDA," Ababu alisema.

Gavana huyo wa zamani alitoa tamko hilo huku kukiwa na shangwe kutoka kwa wakazi ambao walionekana kuunga mkono uamuzi wake.

View Comments