In Summary

•KPLC ilisema baadhi ya maeneo ya kaunti 4 za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na   Nairobi, Kiambu, Siaya na Migori.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Mei 22.

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na   Nairobi, Kiambu, Siaya na Migori.

Katika eneo la Nairobi, sehemu kadhaa za mtaa wa Githurai 45 zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za eneo la Boro katika kaunti ya Siaya pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Vilevile, sehemu kadhaa za maeneo ya Gogo na Macalder katika kaunti ya Migori  zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Wakati huohuo, baadhi ya sehemu za maeneo ya Gitaru na Kanyariri katika kaunti ya Kiambu pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme.

View Comments