In Summary

•“Mimi ni mwafrika na kupitia uzoefu wangu miaka iliyopita, nina uwezo wa kuingia kwenye taasisi na kuibadilisha,” alisema Raila.

•Aliwaambia mawaziri hao jinsi ushirikiano wa kikanda ni muhimu kama nguzo ya kujenga umoja wa bara

KINARA WA UPINZANI RAILA ODINGA
Image: EZEKIUEL AMING'A

Aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga aliwekeza ari na nia yake ya kuwania uenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika mnamo Jumapili katika Mkutano wa Mawaziri wa Amani na Usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)  katika eneo la Zanzibar, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Raila alichukua muda wake kueleza kwa mawaziri wa EAC kwa nini alikuwa anagombea kiti cha Umoja wa Afrika.

“Mimi ni mwafrika na kupitia uzoefu wangu miaka iliyopita, nina uwezo wa kuingia kwenye taasisi na kuibadilisha,” alisema Raila.

Vilevile, aliwaambia mawaziri hao jinsi ushirikiano wa kikanda ni muhimu kama nguzo ya kujenga umoja wa bara hata alipokariri kufaa kwake kuchukua matamanio ya bara kwa kiwango cha juu kuliko ilivyo leo.

“Ninaamini AU ni taasisi yenye inaweza kufanya zaidi kushinda leo. Hiyo ndiyo sababu ninataka kuenda humo,” alisema.

Mbali na hayo, Raila alisema kuwa, iwapo atapata fursa ya kurithi kiti hicho, atajitahidi katika kuleta amani na mikakati ya usalama kwenye bara ambayo alisisitiza ni muhimu katika ukuaji wa bara.

“Hakuwezi kuwa na maendeleo bila amani. AU ina fedha za amani ila amani haijastawi ifaavyo. Baadhi ya mataifa yamechangia ila bado ni kiduchu. Tunahitaji kupanua fedha zetu ili waafrika waweze kukimu uhasama kwenye bara wao wenyewe.”

Kiongozi huyo wa upinzani aliahidi kuzuru tena maazimio yaliyopitishwa na AU yaliyolenga katika kunyamazisha bunduki haramu 2020 ambayo ilisalia kuwa kwenye karatasi.

“Bado kuna bunduki haramu barani. Tunafaa kuona namna tunaweza kutumia fedha za amaniili kuleta amani barani. Hiyo ni mojawapo ya mambo ninataka kukomesha,” aliongeza Raila.

View Comments