logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo, Jumatano

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Murang'a, Meru, Kiambu, Nyeri, Homa Bay, Kakamega, Uasin Gishu.

image
na Samuel Maina

Habari07 August 2024 - 04:27

Muhtasari


  • •KPLC imesema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Murang'a, Meru, Kiambu, Nyeri, Homa Bay, Kakamega, Uasin Gishu.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Julai 25. 

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Murang'a, Meru, Kiambu, Nyeri, Homa Bay, Kakamega, Uasin Gishu.

Katika kaunti ya Kiambu, maeneo ya Ndula, Kolping, Gatuanyaga, Landless na mtaa wa Kisii yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Langas na Kisumu Ndogo katika kaunti ya Uasin Gishu yataathirika kati ya saa nne asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la Meteorological katika kaunti ya Kakamega litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Katika kaunti ya Homa Bay, maeneo ya Kikubi na Nyandiwa yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya Munyange, Miirini, Gituiga, Kiawarigi, na Gitunduti katika kaunti ya Nyeri yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Kiengu, Kinna, na Garbatulla katika kaunti ya Meru yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Nyakianga na Kenya Njeru katika kaunti y Murang'a pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved