logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo, Alhamisi

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Makueni, Kiambu, Nyeri, Kirinyaga, na Busia.

image
na SAMUEL MAINA

Habari04 July 2024 - 04:34

Muhtasari


  • •Kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Makueni, Kiambu, Nyeri, Kirinyaga, na Busia.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Julai 4. 

Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Makueni, Kiambu, Nyeri, Kirinyaga, na Busia.

Katika kaunti ya Nairobi, eneo la Village Market litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Emali na Sultan katika kaunti ya Makueni zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Murera Sisal na Juja Farm katika kaunti ya Kiambu zitashuhudia kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Nyeri, sehemu kadhaa za maeneo ya Ithenguru na Kiandu zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na mbili asubuhi.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kutus na Kagio katika kaunti ya Kirinyaga pia zitakosa umeme kati ya saa mbili unusu na saa tisa unusu alasiri.

Eneo la Mau Mau Market katika kaunti ya Busia pia litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na mbili asubuhi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved