In Summary

• Alisema 2022 alilazimika kumuunga Odinga mkono kwa kuwa ndio ulikuwa uamuzi wa maana kipindi hicho, na kusema hawezi tena.

Kalonzo na Raila Odinga Mkuu wa Azimio la Umoja One-Kenya, Kalonzo Musyoka akiwaonyesha wakuu wachache Raila Odinga jambo kwenye simu yake wakati wa mkutano wa kampeni huko Turkana, Aprili 4, 2022.
Image: TWITTER// RAILA ODINGA

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amesema kuwa sasa ameerevuka na hatoweza kurudia makossa kama aliyofanya mwaka jana kumuunga kinara wa ODM Raila Odinga mkono kwa mara ya tatu.

Akizungumza Jumatano katika kionjo cha mahojiano ya runinga ya NTV ambayo yanatarajiwa kupeperushwa kwa ukamilifu Alhamisi, Musyoka alisema kuwa ujinga ndani yake ulimtuma kumuunga mkono Odinga kwa mara ya tatu, huku akisema kuwa ujinga huo sasa umekwisha.

“Mjinga ndani yangu alimalizia akimuunga mkono Odinga mkono kwa mara ya tatu. Lakini mjinga huyo sasa ameerevuka na hatoweza kurudia makosa kama yale. Ilituchukua muda wa changamoto nyingi kuafikia uamuzi ule na Wakenya wanakumbuka. Niliketi chini na rafiki yangu Raila na kumuonesha kile tulichokuwa tumekubaliana katika maandishi na ilinibidi niiteme na kusema ‘niko tayari kumuunga mkono’ Raila. Kwa wakati huo hicho ndicho kilikuwa kitu cha maana kufanya na kwa hivyo mimi si mjinga,” Kalonzo alisema.

Kiongozi huyo wa Wiper alisisitiza kuwa hii si mara ya kwanza anachafuliwa kwani mara kadhaa amepakwa tope na kuitwa majina tofauti lakini bado yeye yuko na anaipenda Kenya.

Mwishoni mwa mwaka jana, mwandani wa Kalonzo ambaye ni seneta wa Kitui Enock Wambua alisisitiza kuwa mwanzoni mwa mwaka huu walikuwa wanataka kuanzisha mchakato wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya kumtangaza Musyoka kama kinara wake kuelekea uchaguzi wa urais mwaka 2027.

View Comments