In Summary

• "unataka kumwomba mratibu kusitisha maandamano hayo ili wale ambao hawakufungua maduka yao warudi kazini mchana wa leo,” Gachagua alisema.

• Maeneo mengi katika miji ya Kisumu na Nairobi yamesalia mahame tangu alfajiri ya Jumatatu Machi 20 kufuatia tishio la mali kuharibiwa.

DP Gachagua amuomba Odinga kusitisha maandamano.
Image: Facebook, Maktaba

Naibu wa rais Rigathi Gachagua amemlilia kiongozi wa upinzani Raila Odinga kusitisha maandamano akisema kwamba wanachokifanya si vizuri kwa biashara nyingi mijini.

Gachagua alisema kwamba mpaka Jumatatu adhuhuri, nchi ilikuwa imepoteza Zaidi ya bilioni 2 kutokana na biashara nyingi kufungwa kwa kuhofia uharibifu unaotokana na maandamano.

“Tunataka kuwasihi watu hawa wazingatie kusitisha machafuko na vitisho mchana wa leo kwa sababu wanachofanya ni kuharibu uchumi wetu. Matukio yanayoonyeshwa na upinzani si mazuri kwa biashara na uchumi. Tunataka kumwomba mratibu kusitisha maandamano hayo ili wale ambao hawakufungua maduka yao warudi kazini mchana wa leo,” Gachagua alisema.

Gachagua pia alimtaka Odinga kuwa muungwana na kukoma kuwatumia watu aliowataja kama watoto wa maskini katika kushiriki maandamanao hayo ambayo yamelemaza shughuli nyingi katika maeneo mengo ya jiji la Nairobi tangu asubuhi ya Machi 20.

“Tunawaomba wanaoandaa maandamano na fujo wawe watu wenye heshima, hawawezi kuwauliza watoto wa watu masikini wajihusishe na vurugu wakati watoto wao wenyewe wako salama EALA. Sio haki, si sahihi,” DP alilia.

Maandamano ya muungano wa Azimio la Umoja One Kenya yalianza asubuhi ya Machi 20 katika miji ya Nairobi na Kisumu na hali haijakuwa sawa kwani maeneo mengi ya kibiashara yamesalia mahame, maduka yakiwa yamefungwa na uchache wa watu na shughuli za kawaida ukishuhudiwa.

View Comments