In Summary
  • Katibu Mkuu huyo wa zamani wa KNUT aliendelea na kusema hatua za Uhuru zitaathiri utoaji wa huduma kwa utawala uliopo.
Wilson Sossion
Image: KWA HISANI

CAS wa Utalii Wilson Sossion Jumanne asubuhi alisema hatua za Rais wa zamani Uhuru Kenyatta ni aibu kwa eneo na kimataifa kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa mahojiano, alisema anachafua majina ya marais wastaafu.

"Uhuru Kenyatta, kama rais wa zamani, anaweka utangulizi mbaya sana... Ukweli wa mambo unabakia kuwa Uhuru anakuwa aibu ya kikanda na kimataifa," alisema.

Alisema rais huyo mstaafu amekiendesha vibaya chama chake tawala.

"Ilifika wakati aliiacha serikali ya sasa ifanye kazi yake kwani muda wake ulikuwa umepita."

Katibu Mkuu huyo wa zamani wa KNUT aliendelea na kusema hatua za Uhuru zitaathiri utoaji wa huduma kwa utawala uliopo.

"Karibu yuko katika hatua ya kuvuruga utaratibu wa kisiasa wa nchi," alisema.

Sossion alikariri hisia za Waziri wa Ulinzi Aden Duale, ambaye mwishoni mwa juma alisema kwamba hatua za hivi majuzi za Rais huyo wa zamani zilikuwa za aibu.

Matamshi yake Sossion yanajiri siku moja baaa ya rais mstaafu Uhuru kuwafurusha wanachama 10 kutoka Jubilee, huku akiwateuwa viongozi wapya.

Kenyatta alisisitiza mnamo Jumatatu, Mei 22, 2023 kwamba hababaishwi na wanaotaka kumvua taji la uongozi chamani, akisema alivikwa kofia hiyo na wananchi.

Rais huyo wa tano wa Kenya alisema;

“Ningetaka wajue (wapinzani wake); Niliteuliwa na wananchi kuongoza chama, kisha wakanichague hadi nilipoachilia mamlaka na Wakenya ndio wataniondoa katika Jubilee.”

Alitoa matamshi hayo katika Kongamano la Kitaifa la Juibilee, mnamo Jumatatu, Mei 22, 2023 lililoandaliwa jijini Nairobi.

Majuzi, baadhi ya viongozi na wanasiasa wa Jubilee wanaoonekana kuegemea kwa serikali ya Kenya Kwanza walimbandua Kenyatta kutoka kwa wadhifa wake, nafasi yake ikitwaliwa na mbunge maalum Sabina Chege.

Katibu Mkuu wa chama hicho Bw Jeremiah Kioni, pia alivuliwa joho lake aliyekuwa mbunge wa Kieni Kanini Kega akitangazwa kumrithi.

Kenyatta na Kioni, hata hivyo, wakihutubu katika kongamano la Jubilee, walisisitiza kwamba wangali mamlakani.

Kwa upande wake rais huyo mstaafu, alionya wanaomchokoza akidai yeye hatishwi na yeyote.

View Comments