In Summary

•Mnamo Oktoba 5, Bloomberg iliripoti kuwa X ilikuwa inapanga kujaribu viwango vitatu vya huduma ya kulipia kwa watumiaji kulingana na idadi ya matangazo yaliyoonyeshwa.

• X hakubainisha ikiwa sera hiyo hatimaye itatanuliwa kwa watumizi wa X katika nchi zingine.

Elon Musk
Image: GETTY IMAGES

X ya Elon Musk, ambayo awali ilijulikana kama Twitter, imeanza kutoza watumiaji wapya nchini New Zealand na Ufilipino ada ya $1, sawa na shilingi 150 za Kenya kila mwaka ili kutumia jukwaa hilo.

Kwa mujibu wa Business Insider Africa, Sera hiyo, ambayo inaanza leo, iliripotiwa kwa mara ya kwanza na Kylie Robinson wa Fortune siku ya Jumanne.

Ilithibitishwa haraka na jukwaa lenyewe iliposema kwamba ilikuwa ikifanya majaribio mpango wake mpya wa "Not A Bot" katika nchi hizo mbili. X hakubainisha ikiwa sera hiyo hatimaye itatanuliwa kwa watumizi wa X katika nchi zingine.

Kama sehemu ya jaribio, "akaunti mpya, ambazo hazijathibitishwa" zitalazimika kulipa ada ya usajili ya kila mwaka ya $1 "ili kuweza kuchapisha na kuretweet machapisho mengine." Watumiaji waliopo hawataathiriwa na jaribio, jukwaa hilo lilinukuliwa na Business Insider Africa.

Jukwaa liliongeza kuwa sera mpya haikuwa "kiendeshaji faida" na badala yake ilikusudiwa kupunguza ushawishi wa roboti.

Musk na kampuni yake wametafakari kwa muda mrefu kufanya mabadiliko kwenye mipango ya malipo ya jukwaa.

Mwezi uliopita, Musk alimwambia waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, wakati wa mtiririko wa moja kwa moja kwamba X inaweza kuanzisha paywall ya malipo kwa watumiaji wake wote.

"Kwa kweli tutakuja na bei ya kiwango cha chini. Tunataka iwe kiasi kidogo tu cha pesa," bilionea alisema wakati huo. "Ni majadiliano marefu, lakini kwa hakika huu ndio utetezi pekee dhidi ya majeshi ya roboti."

Mnamo Oktoba 5, Bloomberg iliripoti kuwa X ilikuwa inapanga kujaribu viwango vitatu vya huduma ya kulipia kwa watumiaji kulingana na idadi ya matangazo yaliyoonyeshwa.

Musk amefanya mabadiliko mengi kwenye jukwaa tangu alipoipata Oktoba 2022.

View Comments