In Summary

• “Nimekuwa na watu wengi wakiniambia, ‘Wewe ni bikira mpaka umefanya mapenzi na mwanamume,’” msichana mmoja alieleza.

• "Lakini kwa kweli, nimekuwa nikifanya mapenzi na wasichana wenza tangu nilipokuwa na umri wa miaka 15."

Mke aomba kufanya mapenzi na ex kabla kufa
Image: Hisani

Utafiti mpya uliofanywa kwa vijana wa kati ya umri wa miaka 18 hadi 26 nchini Marekani unaonesha kwamba wengi wanatilia shaka dhana ya mtu kuwa bikira kama hajawahi shiriki mapenzi.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na Business Insider, asilimia 56 ya vijana hao walikiri kufanya mapenzi, na hiyo haimaanishi kwamba wao bado ni bikira katika tansiri ya kizamani ya kufikiria pindi unaposikia neno ‘bikira’ likitamkwa.

Vijana hao wanahisi kwamba mtu kupoteza ubikira wake si tu kupitia kuingiliwa kimwili, bali kuna njia nyingi za kuangalia suala la kupoteza ubikira, ikiwemo kutazama filamu za watu wazima, kujichua mwenyewe au hata kufikiria suala na ngono.

"Kuna njia nyingi za kutazama ubikira kama vile kuna njia za kutazama ngono," kijana mmoja aliambia chapisho kwenye mahojiano. "Kinachomaanisha ngono kwa kila mtu kitakuwa tofauti kidogo, haswa kulingana na jinsia yako au mwelekeo wako wa kijinsia."

"Unapoamua kuwa umefanya ngono ... hiyo inategemea mambo mengi ya kijamii na kitamaduni," Kijana mwingine wa Gen Z aliongeza.

Kupoteza ubikira kwa kawaida kumerejelea tendo la kuingiliwa kwa kimwili kutumia sehemu ya uzazi ya kike, lakini kwa kuwa zaidi ya robo ya Gen Z haswa mataifa ya ughaibuni inajitambulisha kama LGBTQIA+, dhana hiyo imekuwa ya utata.

Mwalimu wa jinsia mbili Sasha Roberts, 20, aliiambia Business Insider kwamba amekuwa kwenye "utata wa ubikira" kwa miaka mitano.

Roberts alikuwa akifanya mapenzi na wanawake katika ujana wake na alianza tu kuchumbiana na wanaume mnamo 2022.

“Nimekuwa na watu wengi wakiniambia, ‘Wewe ni bikira mpaka umefanya mapenzi na mwanamume,’” msichana huyo alieleza. "Lakini kwa kweli, nimekuwa nikifanya mapenzi na wasichana wenza tangu nilipokuwa na umri wa miaka 15."

"Je, nyakati hizo zote hazihesabiki?" Aliuliza. "Wanapotea tu?"

"Kila mtu hufanya ngono kwa njia tofauti," Roberts alisema zaidi. "Kila mtu anajitambulisha kwa njia tofauti za jinsia tofauti na kila mtu anaunganishwa kwa njia tofauti sana."

 

View Comments