Matiang'i apondwa Kisii na Nyamira
Matiang’i apondwa na washirika wa Ruto katika ziara ya Nyamira
DP Ruto alikosa kufanya ziara yake katika maeneo hayo wiki jana
- Viongozi hao wamesema hawatotishwa na serikali kuhusu kumuunga mkono Ruto
- Waapa kuendelea na mikutano ya kuwasaidia mahasla
- Wamshtumu Matiang'i kwa kutoisadia jamii ya Wakisii licha ya kuwa madarakani
Washirika wa kisiasa wa naibu wa rais William Ruto wameishtumu serikali kwa kuwatishgia viongozi ambao wanamuunga mkono naibu wa rais William Ruto na kundi lake la ‘Hustler’
Wakizungumza katika hafla iliyohudhuriwa na Ruto huko Nyamira ,mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua alimshtumu waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’I kwa kuwatumia polisi kuwatupia vitoa machozi wafuasi wa Ruto wiki jana akidai kwamba Matiang’i hajaisadia jamii hiyo .
" Ni watu wangapi ambao mtu weni amewasaidia kupata kazi katika serikali ,KWS , magereza na hata uhamasishaji ilhali najiita kiongozi .Maamlaka ni ya muda yatumie kuwasaidia maskini’ amesema siku ya alhamisi
Washirika wa Ruto sasa wanaitaka serikali kuziomba msamaha familia mabazo ziliwapoteza jamaa zao katika machafuko ya Murang’a wiki jana na kuzifidia .
Ruto ameandamana na naibu gavana wa KISII Joash Maangi , Mbunge wa Kitutu Masaba Shadrack Mose, Vincent Kemosi waWest Mugirango, Joash Nyamoko (North Mugirango), na Silvanus Osoro (South Mugirango).
Wengine ni seneta mteule Milicent Omanga, mbunge wa Kiharu Dindi Nyoro, Rigathi Gachagua (Mathira) na mfanyibiashara Don Bosco pamoja na wakilishi wa kauti kutoka Nyamira na Kisii .
Viongozi hao wamesema wanamuunga mkono naiu wa rais William Ruto na vitisho vya serikali havitawatikisa katika msimamo wao huo .
" Kama wabunge na wanachaa wa vugu vugu la hustler ,tupigana kwa kila njia kuhakikisha kwamba unakuwa rais’ amsema mbunge Mose
Mbunge wa North Mugirango Joash Nyamoko amesema naibu wa rais ataendelea kuwasaidia watu ambao ni mahasla nchini
Nyoro amesema washirika wa DP waliondolewa kutoka kamati za bunge kwa sababu ya msimamo wao wa kumuunga mkono .
Alimthubutu waziri wa usalama wa ndani Fred mtaiang’I kumkamata kwa sababu alikuwa katika eneo la Gusii .