Ruto Ziarani Kisii na Nyamira
Wanaojaribu kuzuia mkutano wangu Kisii ni ‘wajinga’-Ruto
Anafanya ziara hiyo baada ya polisi kuwazuia wafuasi wake katika maeneo ya ikutano wiki jana
- Ruto awalaumu baadhi ya watu serikali kwa kuzuia mikutano yake
- Asema hana tatizo na polisi wkani wanafanya kazi kuzilisha familia zao
- Asema hatokoma kuendelea kuwasaidia watu wa kawaida
Naibu wa rais William Ruto amesema maafisa wa polisi ni watu wazuri ambao wanazitafutia familia zao a. Akizungumza huko Nyamira siku ya alhamisi Ruto amesema mkutano wake huo uliofaa kufanyika wiki jana ulizuiwa na baadhi ya viongozi ambao hawajapendezwa na vugu vugu lake la Hasla .
" Hawa pollisi hawana shida . Shida ni watu wanaoishi katika minara mirefu bila kujua shida za watu wengine’ Ruto amesema
Ruto amesema hatozuiwa kuendeea na dhamira yake kusaidia watu wanaofanya kazi katika sekta ya boda boda na biashara nyingine ndogo ndogo .
" Wale wanajaribu kuzuia ziara yangu ya Kisii ni wajinga .watu kama hao ni wakabila . Kila mkenya naruhsiwa kuzuru sehemu yoyote nchin’
Amewarai viongozi kuepuka siasa za kikabila .
" Acheni kuwagawanya wakenya .hakuna mkenya ambaye ni mgeni katika sehemu yoyote ya nchi’
Ruto amesema siasa zinafaa kuwaangazi watu wa kawiada kabla ya kujadili masuala ya siasa za watu kujipa viti na maamlaka .
Amesema serikali ya Jubilee iliundwa ili kuwaunganisha wakenya wote ikiwemo kuwapa nafasi za kazi kwa watu wa Kisii na Nyamira .
Ruto ameandamana na naibu gavana wa KISII Joash Maangi , Mbunge wa Kitutu Masaba Shadrack Mose, Vincent Kemosi waWest Mugirango, Joash Nyamoko (North Mugirango), na Silvanus Osoro (South Mugirango).
Wengine ni seneta mteule Milicent Omanga, mbunge wa Kiharu Dindi Nyoro, Rigathi Gachagua (Mathira) na mfanyibiashara Don Bosco pamoja na wakilishi wa kauti kutoka Nyamira na Kisii . Viongozi hao wameapa kumuunga mkono Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022