Last Updated On 22 October 2020 1 Min Read
Uhuru cheza Jerusalema
Uhuru, Raila wadensi wimbo wa ‘Jerusalema’ katika ziara ya Kisumu
Rais alikuwa ziarani Kisumu
In Summary
- Wimbo wenyewe umewavutia watu muilioni 180 katika Youtube
Rais Uhuru Kenyatta siku ya alhamisi liamua kunengua mauno akicheza wimbo maarufu wa Jerusalema wakati wa ziara yake mjini Kisumu akiwa ameandamana na kiongozi wa ODM Raila Odinga .
Akiwa amevalia shati la rangi ya samawati rais alionekana akipiga mauno kutumia mtindo wake kabla ya Raila kujiunga naye jukwaani pia kucheza .
Gavana wa Kisumu Anyang' Nyongo' na viongozi wengine pia waliingilia kudensi huku wananchi wakiwashangilia . Uhuru alikuwa katika uwanja wa maonyesho wa Mmbo leo ambao sasa umebadilishwa kuwa uwanja wa Michezo .
Wimbo huo wa Master KG na Nomcebo Zikode, umetajwa kama wimbo unaosisimua zaidi baada ya watu wengi sana kuucheza katika nchi mbali mbali na tayari umetazamwa mara milioni 180 katika Youtube .