In Summary
  •  Baadhi ya wazazi wanahofia kuwaruhusu wanao kwenda shule
  • Shule zilitarajiwa kufunguliwa kikamilifu wiki ijayo 

 

Wizara ya elimu imeweka  katika darubuni uwezekano wa kuzifungua kabisa shule na taasisi za masomo

 Wanafunzi wa  Gredi ya nne  4,  darasa la 8  na kidato cha  4  walikuwa tayari wamerejea shuleni wiki mbili zilizopita . Lakini huenda shule  zikafungwa tena kwa  sababu ya kuongezeka kwa visa vya virusi vya corona na wanafunzi  wengine  walitarajiwa kuripoti shuleni jumatatu wiki ijayo.

 Madarasa hayo matatu yanasheheni wanafunzi takriban milioni 2.8

 Arifa ya   muungano wa shule za kimataifa ya tarehe 22 inaonyesha kwamba wizara ya elimu huenda inalenga  kubadilisha tangazo la hapo awali kuwaruhusu wanafunzi wengine kwenda shuleni .

 Wakati wa awamu ya kwanza ya kuzifungua shule  waziri wa  Elimu George Magoha alizitaja siku 14 za kwanza kama  muhimu za kukadiria  iwapo taasisi za elimu ziko tayari kupambana na janga la corona .

 Walimu wakuu waliagizwa kutafuta mianya  na njia za kuisuluhisha .Pia walitakiwa kutathmini mahitaji ya kielimu ya wanafunzi kabla ya kuanza kuwasomesha .

 Lakini maelezo  katika arifa hiyo ya  shule za kimataifa  inaonyesha kwamba serikali huenda inapunguz akasi kuhusu  mpango wake wa kuzifungua shule kikamilifu .

 “ Kwa sababu ya ongezeko la visa vya covid 19  wizara ya elimu  imeamua kuahirisha  kufunguliwa kwa shule’ imesesema sehemu ya arifa hiyo .

 Ongezeko la visa vya covid 19  limeaicha wizaa ya elimu katika njia panda iwapo patahitajika tena kufungwa kwa shule .Duru zaarifu  kwamba pana hofu kuhusu kuendelea kusalia shuleni kwa wanafunzi .

 

View Comments