‘Wenzetu Tanzania hawaulizani kuhusu makabila yao .sisi pia kama wakenya tunafaa kuanza kujitambua kama wakenya na sio wakisii,wakikuyu waluhya ama wajang’o’ amesema Odinga
Akionekana kumkosoa naibu wa rais William Ruto kuhusu siasa za mwaka wa 2022, Odinga amesema viongozi wa Jubilee wanafaa kutekeleza ahadi zao wakati huu na sio kungoja hadi mwaka wa 2022 .
‘Viongozi wa Jubilee wako hapa..mbna ungoje hadi mwaka wa 2022…. Huwezi kuwa na mume kisha mkipata mtoto kichaa unasema mtoto sio wako’ Odinga alisema katika usemi ambao uliwachekesha wajumbe katika ukumbi wa Bomas
Odinga amesema ripoti ya BBI ilikuwa na lengo la kuhakikisha kwamba kuna usawa miongoni mwa jamii za Kenya bali haina lengo la kutumiwa kwa malengo ya kisiasa .