In Summary

 

  •  Sifuna na viongozi hao  wamewataka Uhuru na Raila kuongoza taifa wka kura ya maoni 
  • DP Ruto jumatatu alisema kuna haja ya kutathmini baadhi ya mapendekezo 

 

Vugu vuu moja kutoka  magharibi mwa Kenya limewahimiza rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga  kutokubali marekebisho kufanyiwa ripoti ya BBI na badala yake kuitisha kuandaliwa kwa kura ya maoni .

Magharibi Youth Alliance  ni vugu vugu linalowaleta pamoja viongozi wa vijana kutoka eneo la magharibi  na wamedai kwamba wanaoitisha kurekebishwa kwa ripoti hiyo wana njama ya kusambarataisha mchakato mzima wa kuirekebisha katiba .

 Wakizungumza na wanahabari , wakiongozwa  mbunge wa  Caleb Amisi wa saboti ,  Godfrey Osotsi (mteule)  na katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna  ,viongozi hao wamesema kipindi cha kuirekebisha ripoti ya BBI kimepita  na hatua ifuatayo ya kuandaa kura ya maoni ndio inayofaa kuchukuliwa sasa

 Sifuna amesema muda wa kutoa maoni ulipita kitambo .

" masuala ya  sera yanafaa kuepelekwa katika baraza la mawaziri ilhali ya kisheria yanafaa kupelekwa bungeni ,yale ambayo ynahusu katiba yafikishwe kwa wananchi  kupitia kura ya maoni’ amesema Osotsi .

 Viongozi hao  walikuwa wakijibu  wito wa naibu wa rais William Ruto ambaye siku ya jumatatu alikooa baadhi ya mapendekezo ya  BBI akisema yalifaa kurekebishwa kabla ya kuwasilishwa kwa wananchi kupitia kura ya maoni .

 Ruto  siku ya jumatatu aliratibu hatua kwa  hatua mambo yote katika ripoti hiyo  ambyo anayapiga na yanayostahili kutathminiwa  upya kama ifutavyo;

Idara ya mahakama

 Ruto amesema   kwamba pendekezo la kuundwa kwa afisi ya  kutoa malalamishi kuhusu idara ya mahakama ambayo mshikilizi wake atateuliwa na rais ni jambo am,balo litavuruga uhuru wa idara hiyo .  Ruto amesema hiyo inaweza kulirejesha taifa katika siku za kale ambapo  maamuzi ya majaji yaliamuliwa na rais kupitia simu .

" Tunafaa kuanza kuitumia hazina yay a idara ya mahakama ili iweze kuwaajiri majaji zaidi na kujenga korti katika kila sehemu za nchi kuwahudumia wakeny’ amesema Ruto .

 

Tume ya uchaguzi

 Kuhusu pendekezo la  makamishna wa uchaguzi kuteuliwa na vyama vya kisiasa Ruto amesema hatua hiyo ni kama kuzipa baadhi ya timu maamlaka ya kumteua refarii katika michuano

 “ swali ambalo najiuliza ni je  mchuano kama huo kutakuwa na haki ?’

 Kuhusu kuzuia mshindi katika uchaguzi kuchukua yote Ruto alishangaa jinsi mapendekezo hayo yatakavyozuia hilo ilhali rais ,naibu wake na waziri mkuu na manaibu wake watakuwa kutoka upande mmoja wa kisiasa .

Huduma ya polisi

Ruto, alizungumza kuhusu huduma  ya polisi na kuundwa kwa  baraza la polisi .amesema  katiba ya 2010 iliwapa polisi kuhudumu bila muingilio wowote wa  kisiasa  .

‘Pendekezo la kuwa na baraza la polisi litakaloonozwa na waziri ni kuvuruga uhuru wa polisi’

 Ugatuzi

 Kuhusu  kuongezwa kwa mgao wa fedha za  kauti kutoka asilimia 15 hai 35 Ruto amesema hilo linafaa kuambatana na bunge la senate lenye nguvu . Amesema katika mapendekezo ya BBI senate imepunguziwa nguvu za kuamua kuhusu raslima za kaunti na matumizi yake . Pia amepinga kuondolewa kwa nafasi ya mwakilishi wa akina mama kutoka bunge . Amesema pia kwamba suala la uundaji wa nafasi za ajira na kuboresha biashara ndogo ndoo na za kadri ni jambo linalofaa kutathminiwa upya

 Hotuba ya Ruto kuhusu masuala hayo ya BBI  haikuwapendeza baadhi ya wajumbe katika ukumbi wa Bomas lakini naibu wa rais alisema ana haki ya kuhoji na kuyazua katika mjadala kuhusu njia za kuboresha ripoti hiyo .Baadhi ya wajumbe walianza kumkemea Ruto kwa kelele na akatamatisha hotuba yake kwa kumualika rais Uhuru Kenyatta ambaye alionekana kuiunga mkono ripoti hiyo jinsi ilivyo akisema masuala mengine yanayoonekana kama udhaifu wa ripoti hyo yanaweza kushughulikia mchakato mzima ukiendelea .

 

View Comments