Alishtakiwa kuendesha kliniki bola kibali
Daktari bandia Mugo wa Wairimu ahukumiwa kifungo cha miaka 3 jela
Alidaiwa kuwabaka wanawake baada ya kuwadunga dawa za kulevya
- Mugo sio mgeni wa sakata kama hizo
- Ni mara ya pili anakabiliwa na mashtaka hayo
Daktari bandia Mugo Wa wairimu amepigwa faini ya shilingi milioni 1.4 na endapo atakosa kulipa faini huyo atalazimika kuhudumia kifungo cha miaka mitatu jela kwa kuendesha kituo cha afya bila leseni .
Katika uamuzi wake uliotolewa siku ya jumatano hakimu mkuu mkaazi Martha Nanzushi amesema upande wa mashtaka umethibitisha kesi yake dhidi ya Mugo . pia alishtakiwa kwa kuendesha maabara bila leseni kutoka kwa baraza la wahudumu wa maabara nchini
Wairimu pia alipatikana na hatia ya kuhudumu kama daktari bila leseni .mwaka wa 2018 Wairimu alikanusha mashtaka ya kuendesha kituo cha afya bila leseni na kuhudumu kama muuguzi bila leseni kutoka kwa maamlaka husika .
Muungano wa wauguzi ulijitenga naye ni mara ya pili kwake kutekeleza kosa hilo baada ya kuendesha klini yake mtaani Kayole .
Katibu mkuu wa muungano wa kitaifa wa waugizi Seth panyako amesema Wairimu hayumo katika sajili ya wanachama wao .
Wairimu, alirejea katika vichwa vya habari miaka michache baada ya kumdunga mwanamke mmoja dawa ya kulevya na kisha kumbaka katika kliniki yake isiokuwa na kibali katika mta wa Githurai 44 akihudumu kama mwanajinakolojia