Heroin yanaswa
KRA yanasa Heroin na bangi katika uwanja wa JKIA
Bangi pia ilinaswa
- kumekuwa na ongezeko la visa vya usafirishaji wa dawa za kulevya kupitia JKIA
Halmashauri ya ukusayaji ushuru nchini KRA imenasa Heroin na bangi ambayo ilikuwa ikisafirishwa kupitia uwanja wa ndege wa JKIA .
Dawa hiyo ya heroin ilikuwa ikisafirishwa kutoka Juba ,Sudan kusini na ilikuwa ikipelekwa Cambodia ilhali bangi ilikuwa ikitoka kasese nchini Uganda ikipelekwa nchini ufaransa .
Shehena zote za dawa hizo za kulevya ziligunduliwa wakati wa ukaghuzi katika mashine maalum kwenye uwanja huo wa ndege . Dawa ya heroin ilikuwa imefichwa katika mafungu ya nguo ilhali bangi ilikuwa imefichwa katika mfuko mweusi wa plastiki na kuwekwa ndanio ya nguo ya kitenge .
Wiki moja iliyopita shehena nyingine ya heroine iliyokuwa imefichwa katika mafungo ya nguo ilinaswa ikitoka Juba kupelekwa ufaransa na Cambodia kupitia uwanja wa JKIA .