In Summary

 

  • Oparanya anawaongoza wenzake kwa asilimia 82.3 akifuatwa na gavana wa Kwale Salim Mvurya kwa asilimia 77.
  • Wengine  katika  orodha ya wachapakazi kwa njia bora ni  Anyang’ Nyong’o wa Kisumu kwa asilimia 65.9,Alfred Mutua wa machakos kwa asilimia 65.1, John Lonyang’apuo wa West Pokot kwa asilimia 64.2 , Jackson Mandago wa Uasin Gishu kwa asilimia 63.5

 

Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya Oparanya

 

Gavana wa kakamega  ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya ndiye gavana mchapa kazi Zaidi kuliko wote kwa mujibu wa utafiti wa kura ya maoni uliofanywa na Infotrak .Oparanya anawaongoza wenzake kwa asilimia 82.3 akifuatwa na gavana wa Kwale Salim Mvurya kwa asilimia 77.1, kisha Kivutha Kibwana wa Makueni ni wa tatu kwa asilimia 74..4

 Wengine  katika  orodha ya wachapakazi kwa njia bora ni  Anyang’ Nyong’o wa Kisumu kwa asilimia 65.9,Alfred Mutua wa machakos kwa asilimia 65.1, John Lonyang’apuo wa West Pokot kwa asilimia 64.2 , Jackson Mandago wa Uasin Gishu kwa asilimia 63.5,Njuki Muthomi wa Tharaka Nithi kwa asilimia 62.6 ,Josephat Nanok wa Turkana kwa asilimia 62.5 na Hillary Barchok wa Bomet anafunga kumi bora  kwa asilimia 60.6.

 Katika utafiti huo wanaoshikilia mkia  ni  gavana wa zamani wa Kiambu Ferdinand Waititu ambaye aliondolewa afisini na sasa nafai yake kutwaliwa na  aliyekuwa naibu wake James Nyoro , kwa asilimia 33 ,Moses Lenolkulal wa Samburu kwa asilimia 38.7 Cyprian Awiti wa Homabay kwa asilimia 41.3, John Nyangarama wa Nyamira kwa asilimia 42.5 na  Patrick Khaemba wa Trans Nzoia kwa asilimia 42.7

 Gavana wa Nyeri  Kahiga Mutahi anaongoza kwa magavana wa kaunti za eneo la kati kwa asilimia 56.5,Roba Ali wa Mandera anawaongoza wenzake wa kaunti za kaskazini mashariki kwa asilimia 54.3, naye gavana wa Busia ndiye anayeshika mkia kwa utendakazi miongoni mwa magavana wa eneo la Magharibi kwa asilimia 47.5

 

View Comments