Last Updated On 16 November 2020 1 Min Read
Mahakama
Mwanamume ashtakiwa kwa kuiba shilingi 300,000 katika mkahawa wa McFrys
Kesi itasikizwa tarehe 23 Novemba
Mwanamme mmoja ameshtakiwa kwa kuvamia mkahawa mmoja jijini Nairobi na kuiba shilingi 315,000, simu ya mkononi na masalio ya simu ya shilingi 100
Collins Ouma alifikishwa mbele ya hakimu mkuu wa Kibera Joyce Gandani jumatatu asubuhi .
Ouma anashtumiwa kutekeleza wizi huo juni tarehe 20 mwaka huu katika mkahawa McFrys Hotel Westlands akiwa na wengine ambao hawakuwa kortini .
Kulingana na ripoti ya polisi Ouma alitumia kifunguo cha kujitengezea ili kuingia katika jengo lililo na mkahawa huo na kisha kutekeleza wizi . Hata hivyo amekanusha mashtaka dhidi yake na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tatu pesa taslimu .Kesi hiyo itasikizwa Noveba tarehe 23.