Mahakama

Mwanamume ashtakiwa kwa kuiba shilingi 300,000 katika mkahawa wa McFrys

Kesi itasikizwa tarehe 23 Novemba

Hakimu Mkuu Joyce Gandani

 

 Mwanamme mmoja ameshtakiwa kwa kuvamia mkahawa  mmoja  jijini Nairobi na kuiba  shilingi  315,000,  simu ya mkononi na  masalio  ya simu ya shilingi 100

Collins Ouma  alifikishwa mbele ya hakimu mkuu  wa Kibera  Joyce Gandani  jumatatu asubuhi .

Ouma anashtumiwa kutekeleza wizi huo  juni tarehe 20 mwaka huu katika mkahawa McFrys Hotel Westlands  akiwa na wengine ambao hawakuwa kortini .

 Kulingana na ripoti ya polisi   Ouma alitumia kifunguo cha kujitengezea ili kuingia katika jengo lililo na mkahawa huo na kisha kutekeleza wizi .  Hata hivyo amekanusha mashtaka dhidi  yake na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tatu pesa taslimu .Kesi hiyo itasikizwa Noveba tarehe 23.