Waziri wa Elimu George Magoha

Jaji mmoja ameagiza kufunguliwa kwa shule zote katika 80 zijazo na kupiga marufuku masomo yanayotolewa kijamii yalioanzishwa na serikali .

 Jaji James  Makau  pia amesema waziri wa elimu  George Magoha  hana mamlaka ya  kuagiza kufunguliwa kwa shule chini ya sheria ya elimu ya msingi .

 Jaji amesema waziri  Magoha  anafaa kuhakikisha kwamba shule zinafunguliwa  na kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba kanuni za wizara ya afya kuhusu kuzuia maambukizi ya corona zinatekelezwa .

  Katika uamuzi wake jaji amesema serikali  ilikiuka haki za wanafunzi  na kukosa kuonyesha jinsi masomo ya kijamii yalivyo halali kwa mujibu wa sheria . Uamuzi huo umetokana na kesi iliyowasilishwa na Joseph Enock Aura .

 

View Comments