Jaji mmoja ameagiza kufunguliwa kwa shule zote katika 80 zijazo na kupiga marufuku masomo yanayotolewa kijamii yalioanzishwa na serikali .
Jaji James Makau pia amesema waziri wa elimu George Magoha hana mamlaka ya kuagiza kufunguliwa kwa shule chini ya sheria ya elimu ya msingi .
Jaji amesema waziri Magoha anafaa kuhakikisha kwamba shule zinafunguliwa na kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba kanuni za wizara ya afya kuhusu kuzuia maambukizi ya corona zinatekelezwa .
Katika uamuzi wake jaji amesema serikali ilikiuka haki za wanafunzi na kukosa kuonyesha jinsi masomo ya kijamii yalivyo halali kwa mujibu wa sheria . Uamuzi huo umetokana na kesi iliyowasilishwa na Joseph Enock Aura .