Idara ya DCI imewashauri wazazi kuwa waangalifu kuhusu mienendo ya watoto wao wakiwa nyumbani na wanachofanya mitandaoni
Mkuu Wa DCI George Kinoti amesema wanalisaka genge la wahalifu ambalo linawatumia watoto kufanya vitendo visivyo halali
Kinoti amewaonya wazazi kwamba wanafaa kufuatilia shughuli za wanao mitandaoni pia
" Uchunguzi ukiendelea tungependa pia kuwaonya watu wanaowatumia watoto kutekeleza uhalifu na kujihusisha na vitendo vingine vibaya kupitia mitandao ya kijamii’ amesema Kinoti
Makachero wanalichunguza kundi moja linalotumia mitandao ya kijamii kuwatumia waichana wa shule kujihusisha na uhalifu kama vile kuteneza picha za ponografia na kuwafanya watoto hao kutoweka kutoka majumbani kwa siku kadhaa .
DCI imewaokoa wasichana sita walioripotiwa kupotea baada ya video kusambazwa mitandaoni kutaka maelezo yatakayosaidia warejee nyumbani .
Kulingana na mwanamke mmoja aliyetengeza ombi hilo kupitia njia ya video wasichanahao walitoweka tarehe 14 Novemba baada ya kuhadiwa kutoka makwao na mtu aliyejulikana .wasichana hao saba walikuwa na umri wa miaka 16 kutoka mtaa wa Komarock ,Nairobi