Huduma za Treni
Wakaazi wa Athi River kupata huduma za treni kuanzia jumatatu
Wakaazi wa Athi River sasa wana chaguo la kutumia reli
- Huduma hiyo imezinduliwa maajuzi na rais Uhuru
- Huduma hizo za usafiri zitakuwa zikifanyika kila siku asubuhi na Jioni
Wakaazi wa Athi River kuanzia jumtatu watanufaika na huduma za usafiri wa treni zilizozinduliwa na rais Uhuru Kenyatta wiki jana
Abiria watalipa shilingi 80 kutoka Athi River hadi katika cha Reli cha Nairobi . safari hiyo itachukua muda wa saa moja na dakika 23 kutoka kituo cha reli cha Athi River .
Shirika la Reli siku ya ijumaa limetangaza kwamba treni za usafiri wa abiria zitaanza oparesheni kwenda Athi River siku ya jumatatu na ktoa ratiba ya safari hizo pamoja na gharama yake
Kwa mujibu wa ratiba hiyo treni zitatoka Athi River kila sik asubuhi saa kumi na mbili alfajiri na kusimama Mlolongo saa kumi na mbili na dakika 19 ,imara daima saa kumi na mbili na dakika 52 na makadara saa moja na dakika sita kabla ya kufika CBD saa moja na dakika 23 .
Jioni treni itaondoka kituo cha Central saa kumi na moja na dakika 50 na kusimama makadara saa kumi na mbili na akika tano ,Imara daina saa kumi na mbili na dakika 19 na kufika Athi River saa moja na dakika 13 jioni .
Abiria kutoka CBD watalipa shilingi 50 iwapo watashukia makadara ,shilingi 50 wakishukia Imara Daima,shilingi 60 wakishukia mlolongo na shilingi 80 wakishukia Athi River