In Summary
  •  Barasa amesema ataongoza kampeini za kupinga BBI 
  • Mbunge huyo ameongeza kwamba maoni katika BBI sio ya wakenya wote bali ya wachache 

 

Mbunge wa kimilili Didmus Barasa

 

 Mbunge wa kimilili Didmus Barasa amesema yuko tayari kuongoza kampeini ya kupinga  BBI akiongeza kwamba  mapendekezo katika ripoti hiyo hayasaidia kushughulikia matatizo yanayowakumba wakenya .

Barasa,  ambaye ni mshirika wa karibu wa naibu wa rais William Ruto  ames ema ripoti ya BBI haiwakilishi maoni ya wakenya wengi  kwani haishughulikii masuala kama vile ya ukulima  na kuwalinda wafanyibiashara wadogo wadogo .

" Wakenya wamedanganywa kuamini kwamba unaweza tu kufaulu iwapo mtu wa jamii yako yupo katika nafasi ya juu ya uongozi .Ndio kwa sababu BBI inaongeza nafasi katika serikali  na kuzidisha idadi ya  wabunge’ amesema  Barasa .

" Maoni ya wakenya wote ni muhimu . maoni ya watu waliovalia suti za bei ya juu  sio muhimu kuliko za mama mboga ‘ amesema

Barasa  amesema hataraji kujipata pabaya machoni mwa serikali anapoanza kampeini ya kuwashawishi wakenya kuikataa ripoti ya BBI kupitia kura ya maoni  kwa sababu Kenya ni nchi ya Kidemokarsia

  

View Comments