In Summary
  •    Katibu wa Muungano wa  wauguzi nchini tawi la Mombasa Peter Maroko amesema magavana hawafai kujilinganisha na wahudumu wa afya .
  • " Tunachotaka ni marupurupu ya hali ngumu na hatari  ya kazi yetu  na sio nyongeza ya mishahara kama alivyodai mwenyekiti wa baraza la magavana  Wycliffe Oparanya
Wahudumu wa afya wakiandamana katika barabara ya Nkurumah ,Mombasa

  Wahudumu wa afya Mombasa wanaitaka serikali ya kaunti kukoma kuingiza siasa na ubaguzi katika masuala yao na badala yake kushughulikia mamalamishi waliotoa ili kuboresha sekta ya afya .

 Wahudumu hao wa afya  wamekuwa wakigoma kwa wiki 11  na wamedai kwamba baraza la magavana limekuwa likitoa vitisho kwa wahudumu wa afya ,maafisa wa kliniki na wataalam wa maabara  kurejea kazini  bila  kuongezwa malipo .

   Katibu wa Muungano wa  wauguzi nchini tawi la Mombasa Peter Maroko amesema magavana hawafai kujilinganisha na wahudumu wa afya .

" Tunachotaka ni marupurupu ya hali ngumu na hatari  ya kazi yetu  na sio nyongeza ya mishahara kama alivyodai mwenyekiti wa baraza la magavana  Wycliffe Oparanya

 Amesema kwamba sheria  inahitaji wahudumu wa afya wafidiwe ifaavyo  hasa kwa familia za waleambao waliaga dunia kwa ajili ya Corona wakiwa kazini . Ameongeza kwamba wafanyikazi wengi wa afya wameaga dunia tangu janga la corona kuripotiwa nchini ,hatua inayomaanisha kwamba kazi yao ni hatari .

 

View Comments