In Summary
  •  Katika utafiti wa kura ya maoni uliotolewa na kampuni ya  ,Infrotrak,  takriban nusu ya wakenya  wanasema serikali ilishughulikia  janga la corona kwa njia ya wastani .
  • Asilimia 11 ya wakenya walihisi  wizara ya afya ilikuwa ndio shujaa wao huku asilimia 10 wakimtaja naibu wa rais William Ruto kama shjaa wao .
Rais Uhuru Kenyatta

 Wahudumu wa afya na rais Uhuru Kenyatta ndio mashujaa wa mwaka jana huku Polisi na bunge wakitajwa kama wakiorodheshwa katika nafasi za mwisho .

 Hii ni licha ya wakenya kuitwika lawama serikali ya Jubilee kutokana na jinsi ilivyoshughulikia uchumi wakati wa janga la Corona kwa kuondoa  afueni za ushuru ambazo zilikuwa zimetangazwa na serikali .

 Katika utafiti wa kura ya maoni uliotolewa na kampuni ya  ,Infrotrak,  takriban nusu ya wakenya  wanasema serikali ilishughulikia  janga la corona kwa njia ya wastani .

 

 Kulingana na matokeo ya kura hiyo yaliotangazwa siku ya jumapili  wahudumu wa afya wanashikilia uongozi kwa utendakazi wao  kwa asilimia 76 wakifuatwa na wanahabari kwa asilimia 72 huku mashirika ya kidini yakiwa katika nafasi ya tatu kwa asilimia 65  na rais Kenyatta ni wa nne kwa asimilia 63 .

 Utafiti huo  unaonyesha kwamba asilimia 42 ya wakenya wanahisi kwamba wahudumu wa afya  ndio waliokuwa mashujaa wa 2020 huku asilimia 12 w ya waliohojiwa  wakisema rasi uhuru ndiye shujaa wao .

Asilimia 11 ya wakenya walihisi  wizara ya afya ilikuwa ndio shujaa wao huku asilimia 10 wakimtaja naibu wa rais William Ruto kama shjaa wao .

 Na katika kitakachoikosesha usingizi serikali  takriban thuluthi mbili ya wakenya wanahisi kwamba kuondolewa kwa  afueni za ushuru sio hatua ambayo serikali ilizingatia athari zake kabla ya kuziondoa afueni hizo.

 Idadi kama hiyo inahisi kwamba serikali haikufanya vyema katika kusimamia  uchumi  huku asilimia 30 wakisema wameridhika na jinsi serikali ilivyoendesha uchumi wa taifa .

 Asilimia 45 hawakupendezwa na utendakazi wa polisi  wakifuatwa na bunge kwa asilimia 39 ,senate asilimia 35 na serikali z akaunti kwa asilimia 31.

 Utafiti huo ulifanywa kati ya disemba tarehe 27 na 29 mwaka jana  na uliwahusisha watu 800 walio na umri  wa zaidi ya miaka 18 katika kaunti 24 .

 

  

 

View Comments