In Summary

• Wenyekiti wenza Dennis Waweru na Junet Mohamed walitangaza kuanza kwa mikutano ya kunadi muswada huo juma lijalo.

• Kufikia siku ya Jumatano Musuada huo ulikuwa umepitishwa na zaidi ya mabunge 41 ya kaunti.

Rais Uhuru Kenyatta atia saini wakati wa hafla ya kuzindua saini za kufanikisha ripoti ya BBI. (Picha PSU)

Baada ya muswada wa marekebisho ya katiba 2020 kuafikia vigezo vya kisheria kwa kuidhinishwa na zaidi ya mabunge ya kaunti 24, kamati inayoopngoza mchakato huo siku ya Jumatano ilitangaza kwamba  mikutano ya kupigia debe mswada huo sasa wiki ijayo.

Wenyekiti wenza Dennis Waweru na Junet Mohamed walitangaza kuanza kwa mikutano ya kunadi muswada huo juma lijalo.

Kufikia siku ya Jumatano Musuada huo ulikuwa umepitishwa na zaidi ya mabunge 41 ya kaunti.

 

"Kura ya maamuzi ni kama uchaguzi, lazima tuende nje kufanya kampeni, na tumejiandaa. Katika muda wa wiki mbili au tatu wakati Bunge litakapopitisha muswada huo, tunatarajia tume ya IEBC itupe tarehe ya kura ya maamuzi, ”alisema Junet, ambaye pia ni Mbunge wa Suna Mashariki.

Sekretarieti hiyo iliwashukuru wakilishi wadi katika kaunti zilizoidhinisha muswada huo kuhakikisha kwamba "wanasalia katika mrengo sahihi wa historia."

"BBI ilizaliwa kwa juhudi za kukuza ujumuishaji na kuendeleza uzalendo, wakati wa kujenga Kenya yenye umoja. Tunafurahi kwamba Muswada wa BBI umekubaliwa katika kila mkoa wa nchi hii.

 “Ugatuzi ni nguzo ya Katiba ya 2010 na BBI inataka kuiimarisha kwa kutenga rasilimali zaidi kwa kaunti za kubadilisha maisha ya Wakenya. BBI pia inaimarisha mamlaka ya usimamizi wa Seneti na mabunge ya Kaunti, kama wasimamizi wakuu wa ugatuzi. "

View Comments