Ssebo! Museveni aapishwa kwa muhula wa sita
• Majeshi yalizingira boma la mpinzani wake mkuu Robert Kyangulanyi (Bobi Wine) .
• Hafla ya kuapishwa kwa rais Museveni ilihudhuriwa na marais kadhaa kutoka bara la afrika.
Baada ya uchaguzi uliyosheheni ghasia rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni hatimaye aliapishwa kama rais wa nchi hiyo kwa muhula wa sita wa miaka tano siku ya Jumatano.
Hafla ya kuapishwa kwa rais Museveni ilihudhuriwa na marais kadhaa kutoka bara la afrika.
Huku Museveni akiapishwa mpinzani wake mkuu Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine alisema kupitia mtandao wa Twitter kwamba vikosi vya usalama vilikuwa vimezingira nyumba yake. Kila gari lilokuwa likiingia au kutoka kwake lilikuwa likikaguliwa.
“Hali karibu na nyumba yangu bado ni ya wasiwasi. Makumi ya wanajeshi wamezunguka nyumba yangu, wakikagua kila gari linaloingia au kutoka. Yote hii kukandamiza sauti za raia wakati Kaizari anajivisha taji la 6! nina imani- TUTASHINDA”, Bobi Wine aliandika kwenye Twitter.