Ssebo! Museveni aapishwa kwa muhula wa sita

Muhtasari

• Majeshi yalizingira boma la mpinzani wake mkuu Robert Kyangulanyi (Bobi Wine) .

• Hafla ya kuapishwa kwa rais Museveni ilihudhuriwa na marais kadhaa kutoka bara la afrika.

Baada ya uchaguzi uliyosheheni ghasia rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni hatimaye aliapishwa kama rais wa nchi hiyo kwa muhula wa sita wa miaka tano siku ya Jumatano.

Hafla ya kuapishwa kwa rais Museveni ilihudhuriwa na marais kadhaa kutoka bara la afrika.

Huku Museveni akiapishwa mpinzani wake mkuu Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine alisema kupitia mtandao wa Twitter kwamba vikosi vya usalama vilikuwa vimezingira nyumba yake. Kila gari lilokuwa likiingia au kutoka kwake lilikuwa likikaguliwa.

“Hali karibu na nyumba yangu bado ni ya wasiwasi. Makumi ya wanajeshi wamezunguka nyumba yangu, wakikagua kila gari linaloingia au kutoka. Yote hii kukandamiza sauti za raia wakati Kaizari anajivisha taji la 6! nina imani- TUTASHINDA”, Bobi Wine aliandika kwenye Twitter.

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa miongoni mwa marais waliohudhuria hafla hiyo mjini Kampala.

Rias Uhuru Kenyatta akiwasili mjini Kampala kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais Yoweri Museveni
Rias Uhuru Kenyatta akiwasili mjini Kampala kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais Yoweri Museveni

Viongovi wengine waliohudhuria hafla hiyo walikuwa ni pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania); Sahle-Work Zewde (Ethiopia); Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo); Nana Akufo-Addo (Ghana); Alpha Condé (Gine); Emmerson Dambudzo Mnangagwa (Zimbabwe); Hage Gottfried Geingob (Namibia); Salva Kiir Mayardit (Sudan Kusini) na Mohamed Abdullahi Farmaajo (Somalia).

Rais wa Tanzania Samia Suluhu akishuka kutoka ndege
Rais wa Tanzania Samia Suluhu akishuka kutoka ndege
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo

Rais Museveni ambaye alizaliwa mwaka 1944 katika Wilaya ya Mbarara amekuwa rais wa Uganda tangu mwaka 1986 alipoingia madarakani kupitia mtutu wa bunduki baada ya kupindua serikali ya marehemu Milton Obote.