Wanandoa sasa wako huru kutalikiana kama hisia za mapenzi zimekwisha - Mahakama

Jaji huyo alisema ndoa ambayo mapenzi na hisia zimekwisha toka nje ya mlango wa chumba cha malazi inaweza kuhesabiwa kama ndoa ambayo ilivunjika kitambo, kwani hakuna kingine ambacho kinawashikilia wawili pamoja.

Muhtasari

• Mume huyo alieleza Zaidi kwamba mkewe kwa muda mrefu amekuwa ni mtu wa vimbwaga, mdhulumu na mwenye vurugu kila mara anapoitisha matakwa yake.

Mwanaume na mke wasioelewana kwa ndoa
Mwanaume na mke wasioelewana kwa ndoa
Image: Forbes

Mahakama jijini Nakuru imehalalisha wanandoa kutalikiana kwa kigezo cha kuisha kwa hisia.

Hii ilikuja wakati wa kesi moja ya talaka ambayo hukumu ulitolewa na hakimu Samuel Mohochi, kesi iliyokuwa inawahusu wanandoa wa Kihindi katika mahakama ya Nakuru.

Kwa mujibu wa ripoti, wanandoa hao walikuwa wameelekea mahakamani wakitaka kuachana kwa kigezo kwamba hakukuwa na hisia za mapenzi tena baina yao.

“Hakuna mwanamke au mwanamume ambaye anapaswa kufungwa na sheria za kidini au sheria za nchi wakati hakuna hisia za kimapenzi za kushikilia ndoa pamoja,” jaji Mohochi alisema.

Jaji huyo alisema ndoa ambayo mapenzi na hisia zimekwisha toka nje ya mlango wa chumba cha malazi inaweza kuhesabiwa kama ndoa ambayo ilivunjika kitambo, kwani hakuna kingine ambacho kinawashikilia wawili pamoja.

Kutokana na maelezo hayo, jaji alikubali talaka baina ya mume na mke wake ambao walikuwa wameishi pamoja kwa miaka 20.

Mume katika kesi hiyo alikuwa anadai kwamba mkewe alikuwa anataka maisha ghali licha ya kutoa mchango mdogo katika kusaka utajiri wa familia yao.

Mume huyo alieleza Zaidi kwamba mkewe kwa muda mrefu amekuwa ni mtu wa vimbwaga, mdhulumu na mwenye vurugu kila mara anapoitisha matakwa yake.