Nyota wa zamani wa Chelsea agundua watoto ‘wake’ si wake miaka 12 baadaye

Inasemekana mkewe alidai watoto waliozaliwa Juni 2008 walikuwa wake, jambo ambalo liliwachochea kurasimisha uhusiano wao.

Muhtasari

• Mchezaji huyo wa zamani wa Indomitable Lions, 45, alioa mkewe miaka minne baada ya kuwapokea mapacha hao.

• Hadi uchunguzi wa DNA, mwanasoka huyo aliwalea watoto kama wake.

• "Hakuna watoto ambao wamezaliwa kutoka kwa muungano huu," nyaraka za mahakama zinasema.

Geremi Njitap
Geremi Njitap
Image: HISANI

Ichukuwa miaka kumi na miwili kwa kiungo wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, Geremi Njitap kugundua kuwa watoto mapacha ambao aliamini kuwa alizaa ni wa mume wa zamani wa mkewe.

Vyombo vya habari nchini mwao Cameroon vinaripoti kwamba amewasilisha kesi ya talaka baada ya vipimo vya DNA kuthibitisha ukoo wa watoto hao.

"Hakuna watoto ambao wamezaliwa kutoka kwa muungano huu," nyaraka za mahakama zinasema.

Mchezaji huyo wa zamani wa Indomitable Lions, 45, alioa mkewe miaka minne baada ya kuwapokea mapacha hao.

Inasemekana alidai watoto waliozaliwa Juni 2008 walikuwa wake, jambo ambalo liliwachochea kurasimisha uhusiano wao.

"Lakini ugunduzi kwamba watoto hao walikuwa wa mwenzi wake wa awali uliharibu maelewano ya wenzi hao. Ilimletea mshtuko mkubwa,” stakabadhi za talaka zasema.

Hadi uchunguzi wa DNA, mwanasoka huyo aliwalea watoto kama wake.

Njitap alichezea Real Madrid kati ya Julai 1999, na Julai 2003, alipoondoka na kujiunga na Chelsea katika ligi Kuu ya Uingereza.

Alikuwa na uhamisho mfupi wa mkopo kwenda Middlesbrough kuanzia Julai 2002 hadi Mei 2003 kabla ya kuondoka kwenda Chelsea.

Kiungo huyo aliichezea Chelsea hadi Julai 2007 alipoondoka na kujiunga na Newcastle kwa uhamisho huru.

Aliondoka Newcastle Julai 2010 kujiunga na Ankaragücü kwa uhamisho wa bure na aliondoka klabu hiyo baada ya miezi saba akiwa AE Larisa ambako alikaa hadi kustaafu kwake Januari 2011.