Uchaguzi Senegal: Mgombea urais wa chama tawala akubali kushindwa

Senegal yote inasubiri matokeo rasmi ya muda ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili hii Machi 24, 2024.

Muhtasari

•Mgombea urais na aliyekuwa, Waziri Mkuu wa zamani Amadou Ba ameshangaza kila mtu kwa kutuma pongezi zake kwa Bassirou Diomaye Faye

Image: BBC

Senegal yote inasubiri matokeo rasmi ya muda ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili hii Machi 24, 2024.

Kwa sasa, haya ni matokeo ambayo bado hayajathibitishwa na mamlaka zinazosimamia uchaguzi huo.

Hatahivyo, mgombea wa urais na aliyekuwa, Waziri Mkuu wa zamani Amadou Ba ameshangaza kila mtu kwa kutuma pongezi zake kwa Bassirou Diomaye Faye, mgombea anayeungwa mkono na mpinzani mkuu wa serikali Macky Sall, rais wa zamani wa Pastef Ousmane Sonko.

"Kwa kuzingatia mwelekeo wa matokeo ya uchaguzi wa rais na wakati nikisubiri matokeo kutangazwa rasmi, nampongeza Rais Bassirou Diomaye Faye kwa ushindi wake katika duru ya kwanza," alisema Amadou Ba katika ujumbe uliowekwa wazi.

Anaongeza hivi: “Ninamwomba Mwenyezi ampe nguvu na nguvu zinazohitajiwa ili kushika wadhifa huu mkuu wa ukuu wa nchi yetu. Namtakia mafanikio makubwa kwa ustawi wa watu wa Senegal.”

Kabla ya Amadou Ba, wagombea wengine kadhaa katika uchaguzi huu wa urais tayari wa;ikuwa wametangaza kwamba Bassirou Diomaye Faye ndiye mshindi wa uchaguzi huu.

Wagombea hao ni Pamoja na Khalifa Sall, Anta Babacar Ngom, mwanamke pekee kati ya wagombea 19, Dethié Fall, Thierno Alassane Sall, Mamadou Lamine Diallo.

Mamilioni ya watu walishiriki katika kura ya amani siku ya Jumapili, baada ya miaka mitatu ya machafuko na maandamano ya upinzani dhidi ya Rais anayeondoka Macky Sall.

Matokeo ya kwanza yaliyotangazwa kwenye televisheni yalianzisha sherehe nyingi katika mitaa ya mji mkuu, Dakar. Wafuasi waliwasha fataki, walipeperusha bendera za Senegal na kupiga vuvuzela. Kwa hiyo Waziri Mkuu huyo wa zamani na mgombea wa muungano tawala anafunga orodha ya pongezi zilizotolewa na wagombea waliokuwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi huu