Ndoa yangu ilipovunjika, niligura kanisa la SDA nikajiunga na ulimwengu - Akothee

Mama huyo wa watoto watano alifunguka hayo alipokuwa akizungumza kuhusu safari aliyopitia kabla hajafanikiwa.

Muhtasari

•Akothee amekiri jinsi alivyoacha kwenda kanisa la SDA baada ya ndoa yake kuvunjika takriban miongo miwili iliyopita.

•Baada ya kutengana na Bw Jared, mwimbaji huyo alielekea Mombasa ambako alinuia kujiingiza katika shughuli ya kumpa riziki.

Image: FACEBOOK// AKOTHEE

Mwimbaji Esther Akoth almaarufu Akothee amekiri jinsi alivyoacha kwenda kanisa la SDA baada ya ndoa yake kuvunjika takriban miongo miwili iliyopita.

Mama huyo wa watoto watano alifunguka hayo alipokuwa akizungumza kuhusu safari aliyopitia kabla hajafanikiwa kimaisha.

Alishiriki picha ya zamani iliyomuonyesha akitumbuiza katika klabu moja mjini Malindi mwaka wa 2006 na akazungumza kuhusu jinsi alivyojiachilia baada ya ndoa yake kuisha.

"Unasema ninapokuwa mkubwa, nataka kuwa kama Akothee. Je, umeonja safari ya Esther Akoth Kokeyos kabla ya kuwa Akothee unayemtaka?," Akothee aliandika.

Aliongeza, “Ndoa yangu ilipovunjika, nilitupilia mbali kanisa la SDA na kujiunga na ulimwengu. Sasa nimerudi kanisani 🤣🤣🤣🤣🙏🙏🙏🙏🙏."

 Ndoa ya Akothee na baba ya binti zake wakubwa, Bw Jared Otieno ilivunjwa rasmi Mei 22, 2011, baada ya kesi ya talaka kuwasilishwa 2007. Hii ni baada ya wawili hao kuwa kwenye ndoa rasmi kwa takriban miaka mitano.

Katika mahojiano ya mwaka jana, mwanamuziki huyo wa miaka 43 alidokeza kwamba ndoa yake na Bw Jared iligonga ukuta baada ya baba huyo wa binti zake watatu kumpenda mwanamke mwingine.

Baada ya kutengana na Bw Jared, mwimbaji huyo alielekea Mombasa ambako alinuia kujiingiza katika shughuli ya kumpa riziki.

"Siku zote nilitaka kuwa dereva wa teksi. Sikuwa na karatasi za kwenda kugonga mlango wa mtu, nilikuwa na karatasi za kidato cha 4 tu. (Bw Jared) Alikataa na hati zangu pamoja na kitambulisho changu. Nilipoenda Mombasa singeweza kupata kazi yoyote, hata kuwa mhudumu inahitaji kitambulisho,” Akothee alisimulia.

Ni wakati alipokuwa Mombasa ambapo alikutana na baba yake mtoto wake wa nne ambaye alizaa naye mtoto mvulana wake wa kwanza, Prince Ojwang.

Mwaka wa 2022, Akothee alithibitisha kwamba ndoa yake na Bw Jared Otieno ilivunjwa rasmi mnamo Mei  22, 2011 baada ya kesi ya talaka kuwasilishwa mwaka wa 2007.

Hii ni baada ya kuwa kwenye ndoa halali  na Bw Jared kwa takriban miaka mitano.

"Hati za talaka ziliwasilishwa mnamo 2007, Amri ya Nisi (Kabisa). Kwa hivyo, ndoa hii ilivunjwa mnamo Mei 22, 2011 na Mahakama ya Juu," alisema.