Kajala amuomba msamaha babake Paula, “Wewe ni baba mzuri na nakupenda sana!”

“Kuna vitu vingi sana ambavyo vilikuwa vinaendelea na hakuwa anavipenda kama baba, na mimi nilikuwa najua kabisa kuna vitu nilikuwa navikosea, kwa hiyo ilinibidi kuomba radhi kama mama, ilmradi kila kitu kiwe sawa kwa binti yetu.”

Muhtasari

•  Aidha, kando na kuomba msamaha kwa mzazi mwenziwe, Kajala alimhongera mke mpya wa aliyekuwa mumewe kwa kuwa daraja ya mapatano baina yake na P-Funk.

• “Tunashukuru kwa uwepo wao, na Paul, nisamehe kama nimekukosea kwa vitu vyovyote, na wewe ni baba mwema na nakupenda,” Kajala alisema na kumkumbatia.

Kajala, P-Funk Majani na binti yao Paula
Image: HISANI

Kajala Masanja, mamake Paula ambaye ameolewa na msanii Marioo hatimaye ameamua kuzika tofauti zake na baba wa bintiye ili kufanya kuwa rahisi maisha ya bintiye mbilini.

Kajala na P-Funk Majani, ambaye ni baba wa kumzaa Paula wamekuwa katika mzozo wa muda mrefu, produsa huyo wa zamani akimtuhumu Kajala kwa kila alikuwa anadai ni kumlea bintiye katika misingi mibaya ya kimaisha.

Wakati wa hafla ya kumpokeza Paula zawadi kabla ya kujifungua, wazazi wake wote walihudhuria na Kajala alithibitisha kuwa hawajakuwa katika maelewano mazuri kwa muda na kwamba walikuwa wamepigana block kila mahali mitandaoni na kwenye simu.

“Kuna vitu vingi sana ambavyo vilikuwa vinaendelea na hakuwa anavipenda kama baba, na mimi nilikuwa najua kabisa kuna vitu nilikuwa navikosea, kwa hiyo ilinibidi kuomba radhi kama mama, ilmradi kila kitu kiwe sawa kwa binti yetu,” Kajala alisema.

 Aidha, kando na kuomba msamaha kwa mzazi mwenziwe, Kajala alimhongera mke mpya wa aliyekuwa mumewe kwa kuwa daraja ya mapatano baina yake na P-Funk.

“Kuna vitu nilikuwa nikivizingua yeye anakasirika na Paula anajua kabisa hapa baba amekasirika kwa hiyo anaamua kumtafuta, lakini sisi kimbilio letu lilikuwa ni Samira, mke wa P-Funk, wako miaka mingi na wana watoto 3.”

“Sisi tunampenda kwa sababu, mimi na Paul [P-Funk Majani] tumeblockiana kila mahali kwa ufupi, huwa hatuongei. Lakini nikiona kuna kitu kimefikia shingoni tunahitaji msaada kwa ajili ya Paula nitamfuata Samira na kumuelezea na yeye atafikisha ujumbe na kila kitu kitakuwa sawa,” Kajala alimmiminia sifa mkewe baba bintiye.

Kajala akimalizia alimsifia P-Funk Majani na kusema kwamba yeye ni baba mwema kwa bintiye huku akimkumbatia na kumtaka kumsamehe kwa sekeseke zote ambazo zimetokea baina yao siku za nyuma.

“Tunashukuru kwa uwepo wao, na Paul, nisamehe kama nimekukosea kwa vitu vyovyote, na wewe ni baba mwema na nakupenda,” Kajala alisema na kumkumbatia.