In Summary

• Watoto hao wenye umri wa miaka 12,11 na 9 mtawalia, walikumbana na mauti yao mwendo wa saa tatu asubuhi siku ya Jumapili.

• Watoto hao walikuwa wakichunga mifugo na waliamua kuanza kuogelea katika kidimbwi kilichokuwa karibu.

Mafuriko katika Mto Kawalase - Lodwar
Image: MAKTABA

TAARIFA YA HESBORN ETYANG 

Hali ya simanzi imetanda kwenye kijiji Cha Kanan wadi ya Kanamkemer mjini Lodwar Baada ya watoto watatu kuzama kwenye kidimbwi Cha Maji walipokuwa wakiogelea.

Watoto hao wenye umri wa miaka 12,11 na 9 mtawalia, walikumbana na mauti yao mwendo wa saa tatu asubuhi siku ya Jumapili.

Kulingana na Wakaazi wa eneo hilo, watoto hao walikuwa wakichunga mifugo na waliamua kuanza kuogelea katika kidimbwi kilichokuwa karibu.

Wenyeji  walisema maji kidimbwi hicho hutumika  kuwapa mifugo na kujengea nyumba jambo ambalo wanaomba serikali ya Kaunti ya Turkana kusitisha ili kuepuka visa vya mara kwa mara katika eneo hilo.

Kamanda wa Polisi wa eneo hilo David Mburukwa amethitisha kisa hicho huku mili ya watoto hao watatu  ikipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Lodwar

View Comments