Shughuli ya kuhesabu Kura Juja yasitishwa baada vurumai kuzuka
IEBC yamkashifu Gavana Nyoro kwa kusababisha vurugu
•Kufikia vurugu hiyo, George Koimburi alikuwa anaongoza kwa asilimia sabini na saba.
•Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria adai kunusurika kifo kwa upeo.
Shughuli ya kuhesabu kura katika eneo bunge la Juja imesitishwa kwa muda.
Hii ni baada cha kikundi kinachodaiwa kuongozwa na gavana wa Kiambu James Nyoro kuvamia kituo cha kuhesabu kura cha mang'u na kusababisha vurugu.
Hata hivyo, tume hilo lilitangaza kuwa vifaa vyote na matokeo yaliyokuwa yamefika yako salama. IEBC iliwasihi wagombea kiti wote kuwa wenye utulivu hadi matokeo yatakapotangazwa.
Kufikia kutokea kwa vurugu hiyo, mgombea kiti kwa tikiti ya PEP, George Koimburi alikuwa anaongoza kwa asilimia sabini na saba huku akifuatwa nyuma kwa umbali na Susan Njeri wa Jubilee.
Kupitia ujumbe wa Facebook, mbunge wa Gatundu ya Kusini alieleza masaibu yaliyowakumba wakiwa na Koimburi wakati wa vurugu hiyo."Sasa ni 3.42AM na bado tumekwama katika kituo cha Mang'u. Hatuna uhakika wakati tutakapotoka kwenye kituo hiki. Tunawaomba Wakenya mutuombee. Jana usiku tulinusurika kifo na hiyo ni ishara kuwa Mungu yu nasi" Kuria aliandika.