In Summary

•Ayimba alifariki siku ya Ijumaa baada ya kuuguza matatizo mengi alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya The Kenya Hospital

•Raila Odinga na James Orengo ni kati ya Wakenya waliotuma risala za rambirambi.

Benjamin Ayimba akichezea timu ya taifa
Image: Hisani

Aliyekuwa mchezaji na baadaye kocha wa timu ya raga ya kitaifa, Benjamin Ayimba ameiaga dunia.

Akitangaza kifo chake, msemaji wa familia ya Ayimba, Oscar Osir alisema kuwa Ayimba alikata roho baada ya kuuguza matatizo mengi mwili alipokuwa anatibiwa. Ayimba alikuwa akiuguza ugonjwa wa malaria ya ubongo.

“Familia na marafiki wa karibu wangependa kuwashukuru kwa maombi, ushirikiano na msaada wa kifedha mliojitolea katika siku za Benjamin za mwisho” Osir alisema.

Ayimba alianza uchezaji wa kitaalamu na klabu ya Impala mwakani 1995 baada ya kukamilisha masomo yake katika shule ya sekondari ya Maseno. Ayimba aliongoza timu hiyo kushinda kuchukua ushindi wa Kenyan cup na Enterprise Cup mwakani 2000 na 2001.

Mwanaraga huyo pia aliichezea timu ya Kiingereza ijulikanayo kama Cornish Pirates kati ya mwaka 2003 na 2003.

Aliichezea timu ya taifa ya wachezaji saba na wachezaji kumi na tano kati ya mwaka wa 1997 na 2006. Ayimba alishirikishwa kwenye kikundi cha Kenya 7s kilichocheza kombe la dunia la raga mwakani 2001 na 2005 na kwenye michezo ya commonwealth mwakani 1998, 2002 na 2006.

Baada ya kipindi chake cha kucheza kutamatika, Ayimba alijiunga na ukufunzi huku akifanywa kocha mkuu wa Kenya 7s katika ya mwaka wa 2005 na 2011 na tena mwakani 2015-2016.

Ayimba akiwa kocha wa Kenya 7s
Image: Hisani

Akiwa kocha, aliiongoza Kenya 7s hadi kwenye fainali yake ya kwanza ya kombe la kimataifa iliyofanyika Australia

Pia aliongoza timu hiyo kuchukua kombe lake la kwanza la kimataifa dhidi ya Fiji mwakani 2016 nchini Singapore.

Wakimuomboleza aliyekuwa mmoja wao kwa kipindi kirefu, muungano wa raga nchini(KRU) umesema kuwa Ayimba aliandika vitabu za historia,

“Kama mchezaji, alishinda kila kitu kilichokuwa cha kushindwa nchini” KRU walisema.

Wakenya wa tabaka mbalimbali wameendeelea kumuomboleza na kumsifia marehemu ikiwemo watu mashuhuri kama Raila Odinga, James Orengo kati yaw engine. Hizi hapa baadhi ya jumbe za Wakenya.

Benjamin aliaga akiwa na umri wa miaka 44.
View Comments