In Summary

•Washukiwa hao; Messi Martha Mutioka, Tevin Njuguna, Edward Baraza, Lawrence Gitahi, Kenneth Maina na David Lugali walikamatwa na maafisa kutoka kituo cha Langata katika maeneo ya Kawangware asubuhi ya Jumatano.

•Sita hao si washukiwa wa kwanza kukamatwa maeneo hayo kwa tuhuma za kuibia wasafiri. Jumla ya watu 15 wamekamatwa kuhusiana na uhalifu huo  kufikia sasa .

Washukiwa wa wizi wa simu
Image: Hisani

Maafisa wa polisi wamekamata washukiwa sita  wanaohusishwa na wizi ambao umekuwa ukilenga wasafiri katika barabara ya Southern Bypass.

Maafisa wa DCI wamesema kuwa upelelezi uliofanywa na wapelelezi wa wizi wa mitandao ulisaidia katika kukamatwa kwa washukiwa hao.

Washukiwa hao; Messi Martha Mutioka, Tevin Njuguna, Edward Baraza, Lawrence Gitahi, Kenneth Maina na David Lugali walikamatwa na maafisa kutoka kituo cha Langata katika maeneo ya Kawangware asubuhi ya Jumatano.

Inadaiwa kuwa washukiwa hao wenye umri wa kati ya miaka 21 na 32 wamekuwa wakishambulia waendesha magari na watu wanaosafiri kwa miguu katika barabara ya Southern Bypass.

Simu za rununu mia moja kumi na mbili za aina tofauti ambazo zinatuhumiwa kuwa zimeibiwa ziliweza kupatikana mikononi mwa  washukiwa hao.

Sita hao si washukiwa wa kwanza kukamatwa maeneo hayo kwa tuhuma za kuibia wasafiri. Jumla ya watu 15 wamekamatwa kuhusiana na uhalifu huo  kufikia sasa .

Watu ambao wamepoteza bidhaa za thamani haswa simu wameagizwa kufika katika kituo cha polisi cha Langata ili kuzitambua.

View Comments