19% pekee ya Wakenya wangepiga kura kupitisha BBI iwapo kura ya maoni ingefanyika leo- Utafiti
Utafiti huo ambao ulikamilika Jumatatu umeonyesha kuwa BBI inaungwa mkono zaidi na wanachama wa ODM ikilinganishwa na wale wa Jubilee na UDA
•Utafiti wa hivi karibuni ambao ulifanywa na Tifa umeashiria kuwa asilimia 31% kati ya sampuli ya watu1500 ambao walitumika kufanya utafiti ungepiga kura ya 'La'
Image: Charlene Malwa
Habari na Moses Odhiambo
Wakenya wengi wangepiga kura kupinga mchakato wa BBI iwapo kura ya maoni ingefanyika hivi leo, utafiti umebaini.
Utafiti wa hivi karibuni ambao ulifanywa na Tifa umeashiria kuwa asilimia 31% kati ya sampuli ya watu1500 ambao walitumika kufanya utafiti ungepiga kura ya 'La'
Asilimia kidogo ya 19% wangepiga kura kupitisha mchakato huo, asilimia 18% walisema kuwa hawangepiga kura ilhali 14% hawajafanya maamuzi.
Utafiti huo ambao ulikamilika Jumatatu umeonyesha kuwa BBI inaungwa mkono zaidi na wanachama wa ODM ikilinganishwa na wale wa Jubilee na UDA.
Utafiti huo ulifanywa kwa njia ya mahojiano ya simu kwa watu ambao nambari zao zilichukuliwa kwa njia ya moja kwa moja.
Kiwango cha kosa cha utafiti huo ni +/-2.53%.