19% pekee ya Wakenya wangepiga kura kupitisha BBI iwapo kura ya maoni ingefanyika leo- Utafiti

Utafiti huo ambao ulikamilika Jumatatu umeonyesha kuwa BBI inaungwa mkono zaidi na wanachama wa ODM ikilinganishwa na wale wa Jubilee na UDA

Muhtasari

•Utafiti wa hivi karibuni ambao ulifanywa na Tifa umeashiria kuwa asilimia 31% kati ya sampuli ya watu1500 ambao walitumika kufanya utafiti ungepiga kura ya 'La'

Mchanganuzi wa siasa Tom Wolf akihutubia waandishi wa habari kuhusiana na utafti wa BBI jijini Nairobi mnamo Julai 1,2021
Mchanganuzi wa siasa Tom Wolf akihutubia waandishi wa habari kuhusiana na utafti wa BBI jijini Nairobi mnamo Julai 1,2021
Image: Charlene Malwa

Habari na Moses Odhiambo

Wakenya wengi wangepiga kura kupinga mchakato wa BBI iwapo kura ya maoni ingefanyika hivi leo, utafiti umebaini.

Utafiti wa hivi karibuni ambao ulifanywa na Tifa umeashiria kuwa asilimia 31% kati ya sampuli ya watu1500 ambao walitumika kufanya utafiti ungepiga kura ya 'La'

Asilimia kidogo ya 19% wangepiga kura kupitisha mchakato huo, asilimia 18% walisema kuwa hawangepiga kura ilhali 14% hawajafanya maamuzi.

Utafiti huo ambao ulikamilika Jumatatu umeonyesha  kuwa BBI inaungwa mkono zaidi na wanachama wa ODM ikilinganishwa na wale wa Jubilee na UDA.

Utafiti huo ulifanywa kwa njia ya mahojiano ya  simu kwa watu ambao nambari zao zilichukuliwa kwa njia ya moja kwa moja.

Image: TIFA

Kiwango cha kosa cha utafiti huo ni +/-2.53%.