In Summary
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 188,513  kutoka kwa sampuli 2,012,698
  • Katika visa hivi vipya, 518 ni raia wa Kenya huku 18 akiwa raia wa kigeni, 272 ni wa kiume na 262 ni wanawake
  • Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 4 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 90
  • Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 8.9%
Virusi vya Korona
Image: Hisani

Watu 536 wamepatikana na maambukizi COVID-19 kutoka kwa sampuli 6,036 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 188,513  kutoka kwa sampuli 2,012,698.

Katika visa hivi vipya, 518 ni raia wa Kenya huku 18 akiwa raia wa kigeni, 272 ni wa kiume na 262 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 4 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 90.

Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 8.9%.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 336 wamepona virusi vya corona,236 walipona wakiwa nyumbani huku 100 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 178,119 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 3 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,721 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,092 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 3,982 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 120 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU

 

 

 

View Comments