In Summary

•Kagwe alisema kuwa amri ya kutotoka nje itaendelea kuzingatiwa kutoka saa nne usiku hadi saa kumi asubuhi.

•Serikali pia imetangaza kuwa mikutano yote ya umma na ya ana kwa ana itaendelea kuwa marufuku.

Mutahi Kagwe akitoa hotuba ya kurejelewa kwa mikakati ya kuzuia maambukizi ya Corona
Image: THE STAR

Wizara ya afya imerejelea tena mikakati ya kupambana na janga la Corona nchini.

Kwenye hotuba iliyotolewa na waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe Ijumaa alasiri, baadhi ya mikakati iliyokuwepo itaendelea kuzingatia huku ingine mipya ikitolewa.

Kagwe alisema kuwa amri ya kutotoka nje itaendelea kuzingatiwa kutoka saa nne usiku hadi saa kumi asubuhi.

Watu walio katika kaunti za upande wa ziwa Victoria ambazo zilikuwa zimewekewa amri ya kutotoka nje saa moja ussiku hadi saa kumi kwa sasa wameruhusiwa kuwa nje hadi saa nne usiku.

Serikali pia imetangaza kuwa mikutano yote ya umma na ya ana kwa ana itaendelea kuwa marufuku.

"Kufuatia hayo, mikutano yote ifanyike mitandaoni ama iahirishwe" Kagwe alisema.

Mikutano ya ibada kwenye makanisa, hekalu na mskiti imerushusiwa kuendelea ila kwa kuzingatia mikakati iliyowekwa.

Theluthi moja pekee ya idadi ya waumini ambayo jengo la ibada laweza kusheheni ndio wataruhusiwa kuhudhuria ibada moja kwa wakati.

Waumini pia wanafaa kuzingatia mikakati mingine iliyowekwa kama vile kuvaa barakoa, kukaa umbali wa mita moja na kuosha mikono.

Waziri Kagwe amehimiza waajiri wote kuwakubalisha wafanyikazi wao kuendelea kufanya kazi kutoka nyumbani kama njia moja ya kuzuia maambukizi.

Wizara ya afya imeshauri Wakenya kutojihudumia wakati wanapatikana na matatizo ya kupumua. Wakenya wameshauriwa kutembelea vituo vya afya kila wanapohisi dalili zinazohusishwa na COVID 19.

Hoteli zote zimeagizwa kuendelea kutoa huduma kwa kuzingatia mikakati iliyotolewa na serikali.

Kagwe alisema kuwa serikali inafuatilia ongezeko la visa katika kaunti za Kiambu, Kajiado, Lamu, Makueni, Muranga, Nairobi, Nyandarua , Taita Taveta na Tana River.

View Comments