In Summary

• Kulingana na taarifa ya baraza hilo siku ya Alhamisi kituo hicho kilitoa jukwaa na kuruhusu kupeperushwa kwa ujumbe wa kuudhi mnamo tarehe 9 Oktoba 2021.

Askofu David Ng'ang'a
Image: IVY MUTHONI

Baraza la Vyombo vya Habari nchini Kenya litachukua hatua dhidi ya Sasa TV, baada ya kukamilika kwa taratibu zinazostahili za uvunjaji wa Kanuni za Maadili ya Uandishi wa Habari nchini Kenya.

Kulingana na taarifa ya baraza hilo siku ya Alhamisi kituo hicho kilitoa jukwaa na kuruhusu kupeperushwa kwa ujumbe wa kuudhi mnamo tarehe 9 Oktoba 2021.

Baraza hilo lilisema kwamba Sasa TV ilikiuka kifungu cha 5 (b) (c) cha Uwajibikaji na 10 (1) kuhusu matumizi ya lugha chafu na Ladha katika Kuripoti Kwa kumruhusu mtangazaji, Apostle James Maina Ng'ang'a katika matangazo ya moja kwa moja kwenye kipindi ‘from Jerusalem City Kenya' saa nne na dakika 24 mchana ambapo alitamka maneno ya kuudhi na yasiyofaa kuchapishwa hewani.

Baraza hilo limeagiza Sasa TV kueleza mbona hatua zisichuliwe dhidi yake.

“Tumeagiza kampuni hiyo ionyeshe sababu kwa nini hatua zisichukuliwe dhidi yake, ambapo Baraza litaweka vikwazo vinavyohusika kulingana na mamlaka yetu,” taarifa ya afisa mkuunedatji wa MCK David Omwoyo ilisema.

MCK pia ilisema kwamba inatambua uwezekano wa ukiukaji wa kanuni za redio na televisheni zinazotolewa bila malipo nchini Kenya na limearifu Mamlaka ya Mawasiliano (CA) ipasavyo kwa uchunguzi.

“Tunatahadharisha vyombo vya habari, wahariri, waandishi wa habari na watendaji wa vyombo vya habari dhidi ya kupeperusha maudhui ya kuudhi kwani adhabu kali zitatolewa kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Habari, 2013.

Sasa TV inamilikiwa na mhubiri ambaye si mgeni kwa utata James Ng’anga na kituo cha kuhubiri neon la Mungu.

View Comments