In Summary

• Maafisa hao wa KDF iliripotiwa kwamba walikuwa wakichimba mtaro kuzunguka hifadhi hiyo walipouawa na maharamia.

• Zaidi ya maafisa 20 wa usalama wameuawa na maharamia wa kuiba mifugo katika eneo hilo katika miezi kadhaa iliyopita.

• Hii inafikisha idadi ya maafisa wa KDF walipigwa risasi hadi wanne kufikia Juma Jumatano.

Vikosi vya usalama vimekuwa vikifanya ulinzi wa doria katika maeneo ya Laikipia ili kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi
Image: BBC

Wanajeshi wawili wa KDF na maafisa wawili wa GSU (GSU) waliuawa siku ya Jumatano kwa kupigwa risasi na maharamia waliokuwa wamejihami katika eneo la Kamwenje, Laikipia Magharibi katika machafuko yanayoendelea eneo hilo.

Maafisa wa utawala walisema wengine wanane wakiwemo wanajeshi saba walijeruhiwa katika shambulio hilo la kuvizia lililotekelezwa katika Hifadhi ya Mazingira ya Laikipia (Laikipia Nature Conservancy).

Hii inafikisha idadi ya maafisa wa KDF walipigwa risasi hadi wanne kufikia Juma Jumatano.

Maafisa hao wa KDF iliripotiwa kwamba walikuwa wakichimba mtaro kuzunguka hifadhi hiyo walipouawa na maharamia.

Mauji haya yamesababisha kuimarisha kwa operesheni zaidi katika eneo hilo kuwasaka waliotekeleza shabulio hilo.

Zaidi ya maafisa 20 wa usalama wameuawa na maharamia wa kuiba mifugo katika eneo hilo katika miezi kadhaa iliyopita.

Huku hayo yakijiri Polisi kutoka kitengo cha kupambana na mihadarati wanawashikilia washukiwa watatu baada ya kupatikana wakisafirisha kilo moja ya dawa za kulevya aina ya heroine yenye thamani ya shilingi milioni tatu.

Polisi wanasema washukiwa hao walikuwa wakiendesha shughuli zao kote nchini na kwingineko huku wakijifanya kuendesha biashara halali.

Mmoja wa washukiwa aliyetambulika kwa jina la Swalehe Yusuf Ahmed anafahamika sana kwa ulanguzi wa mihadarati katika eneo la pwani, akiwa tayari anakabiliwa na kesi mbili na amekuwa nje kwa dhamana.

Anahusishwa na ulanguzi wa kilo 105 za heroini zinazokadiriwa kufikia thamani ya shilingi milioni 285.

View Comments