In Summary
  • Watu 11 wanahofiwa kufariki baada ya basi waliokuwa wanasafiria kubingiria kwenye mto Embu
Watu 11 wanahofiwa kufariki baada ya basi kubingiria kwenye mto Embu
Image: Benjamin Nyagah

Watu 11 wanahofiwa kufariki na wengine kadhaa kuachwa katika hali mahututi baada ya basi walimokuwa wamepanda kupinduka na kutumbukia kwenye mto huko Muminje Mbeere Kaskazini katika Kaunti ya Embu.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa eneo hilo Kilonzo Kivinda, idadi ya abiria waliokuwamo bado haijajulikana.

Aliongeza kuwa walionusurika katika ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Siakago Level 4 kwa matibabu.

"Basi hilo linasemekana kubingiria kwenye daraja lililovuka mto. Taarifa za awali zinasema waliothibitishwa kufariki ni 11. Waliopata majeraha mabaya wamepelekwa Siakago Level. 4 Hospitali,” alisema Kivinda.

Basi hilo linaaminika kuwa lilikuwa likiwasafirisha wazee kutoka Mumenje hadi Siakago kwa pesa zao za kawaida za inua jamii

 

 

 

 

 

View Comments