In Summary
  • Kenya siku ya mesajili visa 88 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 4,802 chini ya saa 24 zilizopita
  • Kati ya maambukizi hayo 82 ni wakenya huku 6 wakiwa raia wa kigeni,44 ni wanaume huku 44 wakiwa wanawake
Image: HISANI

Kenya siku ya mesajili visa 88 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 4,802 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 82 ni wakenya huku 6 wakiwa raia wa kigeni,44 ni wanaume huku 44 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,629 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 1.8%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,790,474.

Aidha watu 57 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 247,874,35 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 22 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Hii leo hamna mtu ambaye ameaga dunia kutokana na corona huku idadi jumla ya walioaga dunia ikifika 5,325.

Kuna wagonjwa 367 ambao wamelazwa hospitalini, 993 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 21 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 6,311,035.

 

 

View Comments