In Summary

• Gichovi alisema mwanawe alipenda watoto wake sana na waliishi vizuri kwa amani. Alisema Njuki alikuwa mtoto mzuri na hakutenda maovu alipokuwa anakua.

•Njuki anadaiwa kuua mkewe pamoja na watoto wake kutumia silaha tofauti ikiwemo panga na shoka katika kesi ya ukatili wa kinyumbani.

•Mshukiwa hakusomewa mashtaka dhidi yake , baada ya afisi ya DCI kuwasilisha ombi la kutaka mahakama iwape muda wa wiki mbili ili kukamilisha uchunguzi, ombi ambalo mahakamailikubali.

Paul Murage alipofikishwa mbele ya mahakama ya Gichugu asubuhi ya Jumatano
Image: WANGECHI WANG'ONDU

Njuki Gichovi, Baba ya Paul Murage Njuki ambaye anadaiwa kuua familia yake yote katika kaunti ya Kirinyaga amesema alishangazwa sana na yaliyotendeka.

Akiwa kwenye mahojiano na NTV, Gichovi alisema mwanawe alipenda watoto wake sana na waliishi vizuri kwa amani.

Alisema Njuki alikuwa mtoto mzuri na hakutenda maovu alipokuwa anakua.

“Alikuwa mtoto mzuri na sijawahi kuona kitu kibaya, alikua ni mtoto mzuri sana, sijawahi kumuona akitumia dawa za kulevya na hata sasa alikuwa akilima,” alisema.

"Nimeshtushwa sana na mambo ninayosikia. Aliwapenda watoto wake na waliishi vizuri. Hata walifanya kazi na mke wake."

Njuki anadaiwa kuua mkewe pamoja na watoto wake kutumia silaha tofauti ikiwemo panga na shoka katika kesi ya ukatili wa kinyumbani.

Baada ya kutekeleza  unyama huo siku ya Jumatatu alijisalimisha kwa polisi kisha kuelekeza wapelelezi hadi eneo alikokuwa ametupa silaha za mauaji na nyumbani ambako mili ya wahasiriwa ilikuwa.

Watoto hao ni wa umri kati ya mwaka mmoja na 13.

Polisi walisema mshukiwa aliua watoto wawili wa kiume na binti wawili kabla ya kutupa silaha ya mauaji kwa kichaka kilicho karibu na mto ulio katika kijiji cha Kathata.

Walisema Njuki aliua watoto wawili wa kiume na binti wawili kabla ya kutupa silaha ya mauaji kwa kichaka kilicho karibu na mto ulio katika kijiji cha Kathata.

Wahasiriwa walitambulishwa kama Millicent Muthoni Rungu 38, Nelly Wawira 13, Gifton Bundi Muthoni 13, Sheromit Wambui Muthoni 5, na Clifton Njuki Murage wa mwaka mmoja.

Silaha moja ya mauaji na mkata zilipatikana katika eneo la tukio.

Mshukiwa aliambia polisi alitupa shoka ambayo alitumia kwenye kichaka na msako ukaanzishwa.

Paul Njuki ambaye alifikishwa katika mahakama ya Gichugu hakusomewa mashtaka dhidi yake , baada ya afisi ya DCI kuwasilisha ombi la kutaka mahakama iwape muda wa wiki mbili ili kukamilisha uchunguzi, ombi ambalo mahakamailikubali.

Afisa anayeongoza upelelezi Lazarus Kiprop aliambia mahakama kuwa katika muda wa siku 14, mshtakiwa atafanyiwa uchunguzi wa kiakili ili kubaini iwapo anafaa kujibu mashtaka.

Wapelelezi pia watarekodi maelezo kutoka kwa mashahidi, kukusanya sampuli za DNA kutoka kwa washtakiwa kwa madhumuni ya kulinganisha na vielelezo vilivyo chini ya ulinzi wa mamlaka pamoja na kufanya uchambuzi juu yao.

Pia watafanya msako wa kuwatafuta washukiwa wengine wa mauaji kwa ujumla pamoja na silaha iliyotumika ambayo haipo.

View Comments