Waziri wa elimu George Magoha Ijumaa akiwa katika chuo kikuu cha Kabarak aliwaambia wanafunzi ambao wanajiadaa kukalia mtihani wa kitaifa wa shule ya msingi na ule wa kidato cha nne kwamba mtihani utaendelea kama ilivyopangwa na wizara ya elimu.
Magoha ambaye alikuwa anahotubia wanafunzi wa chuo cha KabaraK ambao walihitimu mwaka huu alitoa dukuduku ambao wanafunzi waliokuwa nao ya mtihani kuharishwa
“ Nataka kutangaza kuwa mtihani uko tayari na utakuwa wa machi... hatutabadilisha kalenda ya mtihani “ alisema Magoha
Isitoshe aligusia mambo na uteketezaji wa shule ambao umekuwa ukiendelea katika maeneo tofauti nchini.
Nakueleza kwamba kitambo mtoto alikuwa wa jamii lakini wakati huu mambo ni tofauti ambapo mtoto anatunzwa bila kurekebishwa
“Wakati wa kitambo watoto walikuwa wa jamii kwa sasa tunaelekea kwa Sodom na Gomorrah mahali ambapo wazazi wanatunza watoto wao kama yai. Tunacho kwa sasa ni watu wakubwa ambao wanaitwa watoto kwa sababu wako shule”